Dodoma FM

Wazazi wametakiwa kuzingatia haki za watoto katika familia

22 July 2021, 8:10 am

Na; Shani Nicolous.

Wito umetolewa kwa wazazi katika jamii kuzingatia haki za watoto wakati wa maamuzi mbalimbali katika familia.

Akizungumza na Dodoma fm msaidizi wa kisheria kutoka Wilaya ya Chamwino Haroni Amos Malima amesema kuwa watoto wanatakiwa kushiriki mambo mbalimbali ya ujenzi wa taifa hata katika familia kwa kusikiliza ushauri wao kwani unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo yakifamilia.

Amesema kuwa pamoja na kwamba watoto hawa wanahaki lakini hawana mamlaka ya kuingilia mali za wazazi wao baada ya utengano hivyo ni vema familia ikatengeneza namna nzuri ya utengano ili kuruhusu sheria kujua namna ya kugawa mali hizo.

Ameongeza kuwa jamii ihamasike katika utoaji wa taarifa za vitendo vya aina yoyote vya kikatili katika vyombo mbalimbaliu vya sheria kutoka ngazi ya kijiji kata mpaka Wilaya .

Amesema wazazi wawalee watoto kwa maadili mema ili kujenga taifa bora na lenye kizazi kilichokuzwa kimaadili ili kutokomeza baadhi ya ukatili unaosababishwa na mila potofu nchini.

AKIZUNGUMZA na dodoma fm hapo jana mkuu wa wilaya ya Chamwino Mh. Gifty Isaya Msuya aligusia suala la kikatili kuwa lipo katika Wilaya ya Chamwino hivyo kama serikali watahakikisha suala hilo linadhibitiwa kwa kuzuia vitendo hivyo ili kuepuka usumbufu wa kesi za kikatili zinazorudisha nyuma maendeleo ya Wilaya.