Dodoma FM

Wakazi wa Ihumwa waelezea imani yao dhidi ya chanjo ya Uviko 19

14 July 2021, 12:16 pm

Na; Victor Chigwada.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Ihumwa Jijini Dodoma wamekuwa na maoni tofauti juu ya dhana ya uchunguzi wa chanjo ya Uviko 19 ambayo bado haijathibitishwa kutolewa hapa Nchinini

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema wamekuwa na wasiwasi juu ya chanjo hiyo kama itatolewa kutokana na kusikia habari zisizo rasmi kuwa kuna madhara yanayo takana na chanjo hizo

Aidha wameongeza kuwa kama Serikali itathibitisha kuwa chanjo hiyo ni salama na haina madhara kwa afya ya mwanadamu watakuwa tayari kupokea chanjo hiyo iwapo Serikali itaruhusu utolewaji wa chanjo hiyo licha ya kuendelea kumuomba mungu

Mwenyekiti wa mtaa wa Ihumwa A Bw. Wiliam Njilimuyi amesema licha ya ugeni wa chanjo hiyo lakini kutokana na kufanyiwa utafiti na mashirika ya afya Duniani hakuna budi wananchi kuunga mkono kama itaanza kutolewa Nchini kwani kinga ni bora kuliko tiba

Naye Dkt. Victor Ngalya kutoka hospitali ya Milembe ameshukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuungana na Dunia katika kufuatilia kwa karibu suala la chanjo ya Corona na kuwasihi watanzania wote kuwa na umoja katika kupambana na wimbi hilo.

Ikumbukwe kuwa Tanzania inaendelea na jitihada za kupambana na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Corona kwa kuwasisitiza wananchi kufuata kanuni zote za kujikinga na janga hilo