Dodoma FM

Wananchi wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufanya utalii wa ndani.

6 May 2021, 11:41 am

Na; Mariam Kasawa

Wananchi wametakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya utalii  wa ndani katika mbuga mbalimbali ili kufahamu vivutio vingi vya utalii vinavyo patikana hapa Nchini.

 Ushauri huo umetolewa na  wawakilishi kutoka hifadhi ya Taifa Tanzania TANAPA wakati wakizungumza na Dodoma FM  juu ya kampeni ya kutembelea mbuga za wanyama msimu wa sikukuu ya Eid .

Bi. Beatrice Mtambi ni Afisa mwandamizi  anaesimamia  masuala ya utalii katika hifadhi ya Taifa ya Tarangire amesema  lengo lao ni kuhamasisha wakazi wa mkoa wa Dodoma pamoja na viongozi kutembelea katika hifadhi za Taifa Tanzania

Bi. Mtambi ametaja gharama watakazochangia watu zitawapatia huduma ya malazi , chakula pamoja na gharama ya gari la kuwatembeza mbugani ambapo amebainisha gharama hizo kama ifuatavyo.

Amewataka wananchi kuacha kuamini kuwa utalii unafanywa na watu wanao toka nje ya nchi  bali wawe na utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii Nchini kwani gharama zake ni nafuu ambazo zinamuwezesha kila mtanzania  kumudu .

Wananchi wametakiwa  watambue kuwa utalii ni jukumu la kila mtu ndani ya Nchi ili kuweza kujifunza  na kuvifahamu vivutio mbalimbali vinavyo patikana ndani ya nchi.