Dodoma FM

Rais Samia akusudia kukutana na viongozi wa kisiasa

22 April 2021, 3:46 pm

Na; Mariam Kasawa.

Rais Samia ameliambia Bunge kuwa anapanga kukutana na viongozi wa kisiasa ili kwa pamoja waweke msimamo wa kuendesha shughuli za kisiasa.

Rais Samia amesema hayo wakati akitaja namna anavyopanga kuboresha mazingira ya uhuru na demokrasia nchini Tanzania.

Amesema “Nakusudia kukutana na viongozi wa kisiasa wa Tanzania, ili kwa pamoja tuweke msimamo wa kuendesha shughuli za kisiasa.”

kupitia hotuba yake Rais Samia Suluhu Hassan ametoa onyo kwa watu wanaofanya ubadhirifu wa mali za umma na kufanya uchonganishi kupitia mitandao ya kijamii.