Dodoma FM

Jeshi la Polisi laendelea kuimarisha ulinzi ndani ya Jiji la Dodoma

2 April 2021, 11:31 am

Na; Mindi Joseph. 

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma limejipanga kuhakikisha linaimarisha ulinzi katika maeneo yote ya nyumba za ibaada ikiwa ni pamoja na kudhibiti uhalifu  katika sikuku ya Pasaka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma Kamanda wa Jeshi la polisi  Mkoani Dodoma Gilles Muroto amesema wameweka askari katika maeneo yote ya nyumba za ibadi ili kuhakikisha sikukuu inafanyika katika hali ya amani na utulivu .

Kamanda Muroto amesema kuwa jeshi la polisi limejipanga pia kuhakikisha hakuna ajali za barabarani zitakazo jitokeza ambazo zitasababishwa na  mwendokasi  pamoja na ulevi.

Wakati huo huo jeshi la polisi linaendelea na Misako mbalimbali ambapo limewakamata watuhumiwa 9 maeneo ya swasawa wanaojihusisha na unyang”anyi na watuhumiwa wawili wa mauji  pamoja na mtu mmoja Leonard Machira mkazi wa kijiji cha Mpwayungu wilayani Chamwino kwa kosa la kumiliki silaha mbili aina ya gobole,ngozi za kenge na dingidingi pamoja na  miche 32 ya bangi aliyopanda nyumbani kwake.

Aidha jeshi la polisi linaendelea kudhibiti uhalifu na watakaobainika kujihusisha  na uhalifu wowote watapelekwa mahakamani.