Dodoma FM

Zoezi la maandalizi lakamilika Jamhuri

21 March 2021, 11:57 am

Na; Mariam Kasawa

Zoezi la kuandaa uwanja wa Jamhuri kwaajili ya kuupokea mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mpaka sasa yamekwisha kamilika .

Akizungumza na vyombo vya habari  Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Patrobas Katambi amesema maandalizi yapo vizuri timu ya mkoa na ofisi ya waziri mkuu inayo ratibu maafa zimejipanga vizuri kuweza kuhakikisha maeneo yote yanakuwa safi na salama ili zoezi hili liweze kwenda vizuri.

Aidha amesema wamehakikisha katika swala la miundombinu kila kitu kipo vizuri ikiwemo  upatikanaji wa maji katika uwanja , taa zipo vizuri  pamoja na  barabara zote zinapitika vizuri.