Dodoma FM

Marais wa nchi 10 kumuaga Magufuli Dodoma

21 March 2021, 10:30 am

Na ; Mariam Kasawa.

Marais  zaidi ya 10 wa Mataifa mbalimbali Duniani wamethibitisha kuhudhuria shughuli ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli itakayofanyika kesho mjini Dodoma.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abasi amesema hadi sasa ana orodha ya zaidi ya marais 10 na ameahidi kuweka wazi majina na nchi zao mchana wa leo.

Rais Magufuli alifariki Dunia Machi 17 kutokana na maradhi ya moyo anatarajiwa kuzikwa Machi 26 nyumbani kwao Chato mkoani Geita.