Dodoma FM

Taasisi zisizo za kiserikali zamlilia Magufuli

19 March 2021, 6:32 am

Na, Alfred Bulahya.

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya MEFADA kwa kushirikiana na YCR (Youth and Community Rehabilitation) zinazojishughulisha na suala la kupambana na dawa za kulevya na ukimwi, imeitaka jamii kuendelea kuenzi mambo muhimu yaliyofanywa na aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt.John Pombe Magufuli.

Akizungumza na taswira ya habari jijini Dodoma mkurugenzi wa taasisi hiyo Bw.Alex Chitawala, amesema hayati Dkt.Magufuli aliongoza jitihada za kupambana na dawa za kulevya na kuonesha matunda ambapo vituo vya kutolea huduma kwa wahanga wa dawa hizo viliongezeka toka vitatu hadi nane .

Aidha Bw.Chitawala amesema Taasisi hiyo imepokea kwa masikitiko taarifa za msiba huo huku akidai kuwa watanzania wanapaswa kushikamana kwa kuwa watulivu katika kipindi chote cha siku za maombolezo kama ilivyoelekezwa.