Dodoma FM

Watanzania wamlilia Rais Dkt.Magufuli

18 March 2021, 7:51 am

Na, Mariam Kasawa.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais Dr John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17 2021.

Akithibitisha kifo hicho makamu wa rais Samia Suluhu amesema kwamba rais Magufuli alianza kuugua mnamo tarehe 6 mwezi Machi na kulazwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya kikwete .

Makamu wa Rais ametangaza siku 14 za maombolezo kwa taifa zima ambapo Bendera zita pepea nusu mlingoti,

Aidha amewataka watanzania kuwa na utulivu pamoja na kuliombea Taifa katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Rais Dr John Pombe Magufuli.