Dodoma FM

Wananchi Matumbulu walilia kituo cha Polisi

29 January 2021, 9:28 am

Na,Victor Chigwada,

Dodoma.

Wananchi wa Kata za Matumbulu na Mpunguzi jijini Dodoma wameiomba Serikali kuwajengea kituo kidogo cha Polisi ili kukabiliana na matukio mbalimbali ya kihalifu.

Wakizungumza na Taswira ya habari wananchi hao wamesema kuwa katika Kata nzima wana askari mmoja pekee hali inayosababisha kutomudu kushughulikia matukio yote yanayotokea.

Bw.Elias Shedrack ambaye ni mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuiomba Halmashauri ya jiji kuwajengea kituo kidogo cha Polisi ili kudhibiti uhalifu.

Akitolea ufafanuzi changamoto hiyo, Diwani wa Kata hiyo Bw.Eliasi Chibago amesema kuwa kwa sasa wanawatumia mgambo kulinda usalama wa raia huku jitihada za kujenga kituo kidogo cha Polisi zikiendelea kwani tayari kuna eneo walishalitenga kwa ajili ya ujenzi.