Dodoma FM

Ntibazonkiza aishuhudia Yanga ikiondoka na pointi tatu

7 December 2020, 9:06 am

Mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari

Dar Es Salaam.

Mshambuliaji mpya wa klabu ya soka ya Yanga Said Ntibazonkiza hapo jana alikaa jukwaani kuishuhudia timu yake ikiibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting.

Ntibazonkiza anatarajia kuanza kuitumikia Yanga kuanzia Sesemba 15 pale dirisha dogo la usajili litakapokuwa limefunguliwa.

Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Burundi alisajiliwa na Yanga wakati alipokuja hapa nchini na timu yake ya Taifa ya Burundi kucheza mechi ya Kirafiki ambayo waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Taifa Stars goli lililofungwa naye Ntibazonkiza.

Yanga imezidi kujikita kileleni mwa ligi kuu Tanzania Bara baada ya ushidi wa jana imefikisha pointi 34.