Dodoma FM

Vieira atimuliwa Nice

5 December 2020, 10:50 am

Patrick Vieira

Nice,

Ufaransa.

Klabu ya Nice imemfuta kazi kiungo wa zamani wa Ufaransa na Arsenal, Patrick Vieira kama kocha wao Mkuu baada ya miaka miwili na nusu ndani ya Klabu hiyo ya Ligue 1.
Klabu hiyo ya Ufaransa imepoteza michezo mitano mfululizo, pamoja na kichapo cha 3-2 Siku ya Alhamisi mbele ya Bayer Leverkusen ambacho kilithibitisha kuondolewa kwao Kwenye Europa League, na ni ya 11 kwenye msimamo wa Ligue 1.
Vieira, ambaye pia alichezea Manchester City, Inter Milan na Juventus, alikuwa kocha wa New York City kabla ya kujiunga na Nice… Adrian Ursea, ambaye alikuwa msaidizi wa Vieira, amechukua jukumu kama kocha mkuu.