Dodoma FM

Dodoma Jiji Fc yajipanga kibabe kuwakabili KMC leo

4 December 2020, 8:25 am

Benchi la ufundi la timu ya Dodoma Jiji Fc

Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji FC Renatus Shija amesema watatumia dirisha dogo la usajili kuboresha baadhi ya nafasi katika kikosi chao ambazo zimeonekana kupwaya.

Shija ambaye timu yake itashuka dimbani hii leo kuvaana na KMC Fc katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam amesena kuwa kuna baadhi ya nafasi zimekuwa na mapungufu hususan katika eneo la umaliziaji.

Kuhusu mchezo wa leo amesema “Lengo letu ni kupata pointi tatu kwenye mchezo wa leo dhidi ya KMC FC ili kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi bila kusubiri kupambana kujinasua kushuka daraja”.