Dodoma FM

SUMA JKT yazindua mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege

25 May 2023, 4:37 pm

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele akizungumza katika uzinduzi huo. Picha na Alfred Bulahya.

Amewaagiza watendaji wa SUMA JKT kuhakikisha wanasimamia mitambo hiyo ili ilete tija iliyokusudiwa katika kuongeza ufanisi wa SUMA JKT.

Na Alfred Bulahya.

Jeshi la Kujenga Taifa kupitia SUMMA JKT, limezindua rasmi mitambo mikubwa ya kuzalisha na kusafirisha zege yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.349 za kitanzania itakayokuwa ikitumiwa kuzalisha zege.

Akizungumza katika eneo la Kisasa jijini Dodoma mara baada ya kuzindua mitambo hiyo Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema kuwa uzinduzi wa mtambo huo unakwenda kuiwezesha SUMA JKT, kuondokana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kununua zege, kukodi magari na kuzisafirisha kwenye miradi yake mbalimbali.

Sauti ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JK.
Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyoni. Picha na Alfred Bulahya.

Aidha amewaagiza watendaji wa SUMA JKT kuhakikisha wanasimamia mitambo hiyo ili ilete tija iliyokusudiwa katika kuongeza ufanisi wa SUMAJKT.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyoni,amesema mitambo hiyo imeingizwa nchini Januari 16, 2023 na kumaliza kusimikwa May 22, 2023 jijini Dodoma.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ujenzi SUMA JKT.