Dodoma FM

Kuandika wosia si kujitabiria kifo

22 January 2023, 10:27 am

Na; Mariam Kasawa.

Wazazi wamekumbushwa kuwa na utamaduni ya kuandika wosia ili mgawanyo wa mali usilete shida endapo mzazi huyo atafariki.

Akizungumza na Dodoma Tv mwanasheria kutoka chama cha wanasheria wanawake TAWLA bi. Neema Ahmed amesema wazazi wanapaswa kujua kwamba kuandika wosia sio kujichulia kifo huku akisisitiza kuwa wosia unaweza kubadilika.

Wakili. Inaelezwa kuwa Wosia unapo andikwa mapema husaidia familia nyingi kuepuka migogoro endapo kutatokea mgawanyo wa mali hizo huku jamii ikikumbushwa kuacha kuwa na Imani potofu dhidi ya kuandika wosia