Dodoma FM

Wakazi jijini Dododma wafurahishwa na msamaha wa riba ya kodi ya Pango

21 October 2022, 10:18 am

Na; Mariam Matundu.

Kufuatia Rais Samia Suluhu Hassan kutoa msamaha wa riba ya kodi ya pango la ardhi uliotolewa kuanzia mwezi julai hadi Desemba mwaka huu ,wananchi jijini Dodoma wameoneshwa kufurahishwa na hatua hiyo.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao Wamesema licha ya furaha yao juu ya Msamaha huo lakini Upo  uzembe na upuuziaji wa vitu hali inayowafanya wananchi kulimbikiza kodi   kwa muda mrefu .

.

Mzee baharia ni mkazi wa mtaa wa majengo  jijini Dodoma amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu anayekutana na changamoto ya kusahau na kujikuta hajalipa kodi hiyo hata kwa miaka 3 na kuiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwakumbusha kwa njia ya ujumbe mfupi kwa simu na kupitia kwa watendaji wa mitaa.

.

Akizungumza katika kipindi cha the morning power hii leo afisa ardhi mteule mkoa wa Dodoma Letare Shoo amesemea kuwa wananchi wengi wanashindwa kutofautisha kati ya kodi ya jengo na kodi ya pango la ardhi ndio sababu ya wengi ulimbikiza madeni , hivyo amewataka wananchi kusikiliza vyombo vya habari ili kupata elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara .

.

kufuatia wananchi wengi kuwa na malimbikizo ya kodi la pango la ardhi Rais Samia ametoa msamaha huo wa riba kwa watu wanaodaiwa kwa kipindi cha miaka mitano na kuendelea .