Dodoma FM

Sherehe za mashujaa kitaifa kufanyika Jijini Dodoma

21 July 2022, 2:17 pm

Na;Mindi Joseph.

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi Katika Sherehe Za Mashujaa Ambayo Kitaifa Yatafanyika Jijini Dodoma.

Akizungumza Katika Viwanja Vya Mashujaa Ambapo Sherehe Hizo Zitafanyika Mkuu Wa Mkoa Wa Dodoma Antony Mtaka Amesema Kuwa Maandalizi Yanaenda Vizuri Na Kamati Ya Ulinzi Na Usalama Imeridhishwa Na Maandalizi Hayo.

.

Aidha Amesema Kuwa Tarehe 24 Usiku Saa Sita Kamili Uongozi Wa Mkoa Na Viongozi Mbalimbali Watakuwa Katika Viwanja Hivyo Kwaajili ya Zoezi La Kuuwasha Mwenge Kuamkia Siku Ya Mashujaa Kitaifa Siku Ya Tarehe 25 Ndio Siku Ya Mashujaa Usiku Saa Sita Kamili Mwenge Huo Utazimwa Katika Viwanja hivyo na kuongeza Kuwa Mkoa Upo Tayari Kuhakikisha Eneo Hilo La Mashujaa Linakuwa Hai.

.

Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Maadhimisho Taifa Ofisi Ya Waziri Mkuu Bathilomeo Jungu Amesema Kuwa Maandalizi Yanakwenda Vizuri Kwani Eneo Hilo Halikuwa Katika Hali Nzuri Na Kazi Ya Ukarabati Wamewakabidhi Suma Jkt Ili Kuhakikisha eneo hilo Linakarabatiwa Na Kuwa Katika Hali Nzuri.

Clip3..Mwenyekiti

Maadhimisho Ya Siku Ya Mashujaa Kitaifa Yatafanyika Tarehe 25 Mwezi Huu Katika Viwanja Vya Mashujaa Jijini Dodoma.