Dodoma FM

Wauguzi na wakunga waaswa kuepuka kupokea rushwa

4 July 2022, 1:15 pm

Na; Benard Filbert.

Wauguzi na wakunga wameaswa kuepuka kupokea rushwa katika maeneo yao ya kazi na kuwahudumia wagonjwa kwa uaminifu ili kulinda na kutunza heshima ya taaluma hiyo.

Hayo yameelezwa na Jane Mazigo mkuu wa idara ya usajili na maadili kutoka baraza wa wauguzi na ukunga wizara ya afya wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha the morning power show.

Amesema kuwa wauguzi na wakunga wanapaswa kuhakikisha  wanapoenda kuripoti sehemu zao za kazi wanachukia rushwa na kukemea na kutokuwa sehemu ya rushwa.

.

katika hatua nyingine amewahimiza wauguzi na wakunga kuomba usaidizi ili huduma iwe bora na salama kwa wananchi wanaowahudumia na kuhakikisha masilahi ya wangonjwa yanakuwa ya kwanza.

.

wauguzi na wakunga  wamewataka kutekeleza imara  mipango ya wizara ya afya na kuelimisha jamii kuhusiana na umuhimu wa sensa.