Dodoma FM

Chimagai waanzisha shule shikizi ili kunusuru elimu ya watoto wao

21 June 2022, 2:45 pm

Na; Victor Chigwada.

Umbali wa shule mama katika kata ya kimagai umewalazimu wananchi kuunganisha nguvu na kuanzisha shule shikizi kwaajili ya watoto wasioweza kutembea umbali mrefu

Hayo yamethibitishwa na Diwani wa Kata ya Kimagai Bw.Noha Lemto amesema changamoto hiyo ya umbali mrefu umepelekea kupoteza watoto na kuiomba Serikali kuzisajili kwa haraka

Lemto amesema  kuwa licha ya umbali huo lakini bado Kuna mto kubwa ambao ukijaa inawalazimu wanafunzi kukaa nyumbani zaidi ya miezi sita kusubir maji kupungua

.

Aidha ameongeza kuwa baada ya kutenganishwa kwa kata walio kuwa wakiitika  Lupeta hapo awali hivyo sekondari kubaki kata hiyo na wao kubaki bila sekondari

Bw.Lemto ameongeza kuwa changamoto ya umbali wa sekondari imekuwa changamoto kwa watoto wa kike na kukatisha ndoto zao kwani maisha ya kujitegemea na kujiendesha wao imekuwa Ni vigumu

.

Mazingira Bora na rafiki kwa mtoto wa kike Ni muhimu ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kimaisha