Dodoma FM

Makaa ya mawe yatapunguza kutoweka kwa misitu

18 May 2022, 2:02 pm

Na;Mindi Joseph.

Shirika la utafiti wa viwanda limefanya utafiti wa matumizi ya Mkaa wa makaa ya mawe utakaotumika nyumbani ili kusaidia kupunguza utowekaji wa misitu.

Taswira ya habari imezungumza na Mtafiti kutoka shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda Tazania Esther Lazaro ambaye amesema wanafanya tafiti bora katika nishati kutokana na uwepo wa changamoto ya matumizi ya  nishati mbadala hususani mkaa unaotokana na makaa ya mawe.

Ameongeza kuwa wanaendelea kuhakikisha jamii inapata uelewa zaidi juu ya matumizi ya mkaa huo unaotokana na makaa ya mawe.

.

Katika hatua nyingine amesema  wanawafikia watazania kwa wakati mmoja na kujenga uelewa kuhusu uvumbuzi na ubunifu.

.

Pamoja na Serikali kuwa mstari wa mbele katika kampeni ya matumizi ya nishati mbadala kama makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia na kupunguza utowekaji wa misitu, lakini bado Watanzania wengi wana uelewa mdogo juu ya nishati hiyo.