Dodoma FM

Wakazi wa Hombolo wauomba uongozi wa kata kuimarisha utunzaji mazingira mnadani

10 August 2021, 12:15 pm

Na;Mindi Joseph .

Wananchi wa vijiji vinavyozunguka mnada wa Hombolo mkoani Dodoma wameomba uongozi ngazi ya kata kuwasogezea huduma ya vyoo pamoja na kuweka usimamizi madhubuti wa utunzaji wa Mazingira mnadani hapo .

Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamebainisha kuwa utunzaji wa mazingira ni kipaumbele cha muhimu hivyo ni vyema uongozi wa kata ukaweka msukumo zaidi wa utunzaji mazingira mnadani hapo ikiwemo kujenga choo na vitunzia takataka kutokana na idadi ya watu kuwa kubwa siku za mnada.

Clip1..Wananchi

Diwani wa kata ya Hombolo Bwawani,Ased Matayo Ndajilo amesema mnada huo huwa unaingiza mapato kwa serikali zaidi ya laki 8 hadi milioni 1 hivyo serikali ya kata imeshaanza ujenzi wa vyoo huku akikiri uchafuzi wa mazingira unavyotokea kipindi cha mnada.

Clip2..Diwani

Mnada wa Hombolo mkoani Dodoma ulianzishwa mwaka 1974 ambapo umekuwa kiungo muhimu cha uchumi kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma na mikoa jirani.