Dodoma FM

Bendera za UN kupepea nusu mlingoti

23 March 2021, 11:36 am

Na; Mariam Kasawa.

Umoja wa Mataifa (UN) umesema Bendera ya Umoja huo itapepea nusu mlingoti katika Ofisi za Makao Makuu jijini New York Nchini Marekani.

 Bendera hiyo itapepea Machi 26, 2021 ili kumuenzi Rais John Magufuli ambaye atazikwa siku hiyo wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Ofisi zote za umoja wa Mataifa  Duniani zimetakiwa kushusha Bendera nusu mlingoti siku hiyo ya maziko ya rais Magufuli.