Dodoma FM

Chuo kikuu Dodoma (UDOM) waikumbuka misingi iliyo jengwa na Rais Magufuli

20 March 2021, 11:41 am

Na, Mariam Kasawa.

Wanafunzi wa chuo kikuu Dodoma ( UDOM) wamesema wanatarajia misingi imara katika Elimu iliyo wekwa na Hayati rais Dkt John Pombe Magufuli itaendelea kuimarika.

Wakizungumza na Dodoma fm wanafunzi hao wamesema wamepokea msiba huu kwa majonzi makubwa kwani rais alikuwa katika kasi ya kulipeleka Taifa la Tanzania katika maendeleo.

Wamesema misingi ya uongozi aliyo ijenga katika vyuo vikuu imesaidia kuondoa migogoro, pamoja na  migomo hivyo kupelekea  wafanyakazi wa vyuo vikuu kufanya kazi kwa weledi.

Stanslaus Sekulu ni mwanafunzi wa project planning and management chuoni hapo yeye anasema Rais alisaidia upatikanaji wa mikopo uwe rahisi tofauti na kipindi cha nyuma hivyo wanaamini utaratibu huo utaendelea ili kuepusha migogoro .

Aidha wanafunzi hao wamesema wanaendelea kumuombea rais Magufuli apumzike kwa amani na wanaamini viongozi waliobaki wataendeleza haya yaliyo achwa , pia wamewaomba wananchi waendelea  kuwa na umoja pamoja na kuliombea Taifa.