Joy FM

Mabinti wanaobeba ujauzito katika umri mdogo wasinyanyapaliwe Kigoma

16 November 2026, 14:20

Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa katika mafunzo malezi ya watoto, Picha na Prisca Kizeba

Katika jamii zetu, kumekuwa na tatizo la baadhi ya wasichana kupata mimba wakiwa na umri mdogo jambo hili limekuwa likisababisha changamoto nyingi katika maisha yao, ikiwemo kukatishwa masomo, kukosa matumaini na kunyanyapaliwa na watu wanaowazunguka na hivyo ni muhimu kuelewa kuwa wasichana hawa hawapaswi kunyanyapaliwa, kudharauliwa wala kutengwa na jamii

Na Prisca Kizeba

Wazazi na Walezi Katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameaswa kutowanyanyasa na kuwanyanyapaa mabinti wanaopata ujauzitio katika umri mdogo.

Hayo yamebainishwa na Mwezeshaji wa huduma ya mtoto upande wa Kigoma Kaskazini na Kasulu  Emmanuel Sota wakati akizugumza na wazazi katika kituo cha Compation kilichopo Mwasenga Manispaa ya Kigoma ujiji

Amesema  wazazi wana jukukumu la kumlinda mtoto wa kike anapopata ujauzito kwa kumwelekeza na sio kumnyanypaa na kumfanyika ukatili wa kumfukuza au kumtelekeza

Baadhi ya wazazi waliokuwepo katika kituo hicho  wamekuwa na haya ya kueleza kuhuhu swala zima la malezi hasa kwa watoto wa kikike wanaopata ujauzito katika umri mdogo