Joy FM

RC Sirro azitaka halmashauri kusimamia miradi kikamilifu

21 August 2026, 16:14

Mkuu wa Mkoa Kigoma akiwa na viongozi mbalimbali katika ukaguzi wa miradi Wilayani Kibondo, Picha na Mwandishi wetu

Usimamizi wa miradi na kuikamilisha kwa wakati husaidia kuanza kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amezitaka Halmashauri Mkoani humo kuendelea kuzingatia usimamizi wa miradi na kuikamilisha kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa

Balozi Sirro amesema hayo akiwa wilayani Kibondo katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambayo itapitiwa na mbio za mwenge mwezi septemba,2026.

Mkuu wa Mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro akipata taarifa za utekezaji wa miradi, Picha na Mwandishi wetu

Amesema matarajio ya serikali pamoja na wananchi ni kuona miradi ikitekelezwa katika viwango vinavyotarajiwa na kukamilika kwa wakati

Aidha Balozi Sirro ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kibondo kwa usimamizi wa miradi ulio thabiti kulingana na thamani ya kila mradi.

Mkuu wa Mkoa Kigoma akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani Kibondo, Picha na Mwandishi wetu

Naye mkuu wa wilaya ya Kibondo Kanali mstaafu Aggrey Magwaza amesema umeshauri ambao umetolewa na mkuu wa mkoa Balozi Sirro watauzingatia na kuboresha mahali ambapo patakuwa na mapungufu