Joy FM

Shule ya wasichana Mkugwa yakabiliwa na upungufu wa nyumba za walimu, mabweni

19 March 2024, 10:02

Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya waschana ya Mkugwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Kibondo Dkt. Florence Samizi, Picha na James Jovin

Shule ya Sekondari ya wasichana Mkugwa iliyoko Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu, mabweni na madarasa hali inayozorotesha kiwango cha taaluma shuleni hapo. 

Hayo yamebainishwa na mkuu wa shule hiyo mwalimu Martha Kajoro wakati akitoa taarifa mbele ya mbunge wa jimbo la Muhambwe Dkt. Florence Samizi wakati akikabidhi vitanda kwa ajili ya wanafunzi shuleni hapo.

Aidha ameitaka serikali kuangalia namna ya kupunguza changamoto hizo zinazoikabili shule ya sekondari Mkugwa hali itakayosaidia kuongeza kiwango cha taaluma shuleni hapo na kuwasaidia wanafunzi wa kike kufikia malengo yao.

Sauti ya Mkuu wa shule ya Mkugwa

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Muhambwe Dkt. Florence Samizi amesema kuwa katika kutatua ama kupunguza changamoto hiyo zaidi ya shilingi milioni 600 zimetumika kukarabati shule hiyo huku mbunge huyo akitoa shilingi milioni 3 kwa ajili ya vitanda vya wanafunzi.

Mbunge wa Jimbo la Mhambwe Dkt. Florence Samizi akiwa na wanafunzi wa Mkugwa Wilayani Kibondo, Picha na James Jovin

“serikali inaendelea kukukisha inaboresha miundombinu ya elimu na lengo ni kuhakikisha mtoto wa kitanzania anapata elimu nzuri na yenye kuwasaidia vijana wa kitanzania na sisi kata wawakilishi wa wananchi tatahakikisha tunawasemea wananchi ili huduma ziweze kutolewa kwa ufasaha”