Joy FM

Wananchi waipa kongole serikali kwa ujenzi wa madaraja ya mawe

6 October 2023, 08:01

Wajumbe wa mfuko wa bodi ya barabara wakikagua daraja la mawe lililojengwa katika kijiji cha Bitale. Picha na KGPC

Teknolojia ya ujenzi wa madaraja kwa kutumia mawe imetajwa kuwa mkombozi kwa wananchi wa wilaya za Kigoma baada ya kurahisisha shughuli za usafirishaji.

Na. Tryphone Odace

Wananchi wa vijiji vya Nyamidaho, Bitale Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Nyamihanga wilaya ya Buhigwe  wameanza kusafirisha mazao yao kupeleka katika masoko mbalimbali mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa madaraja matatu ya mawe yanayokadiriwa kuwa na dhamani ya zaidi ya milioni 300 ambayo yanaunganisha vijiji vyao na barabara kuu ya kuelekea Kigoma mjini.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi ya mfuko wa barabara mkoani Kigoma yenye lengo la kukagua miundombinu ya barabara maeneo ya mjini na vijijini.

Wajumbe wa bodi ya mfuko wa barabara mkoani Kigoma

Wakazi wa vijiji hivyo wanaeleza changamoto yao ya awali kabla ya kupata daraja kuwa walishindwa kusafirisha mazao ambayo wanalima kutokana na kukosekana kwa daraja la uhakika na hivyo kuishia kuuza mazao hayo kwenye masoko yaliyopo vijiji jirani.

Muonekano wa barabara yenye daraja lililojengwa kwa mawe Wilayani Kigoma, Picha na KGPC.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA mkoa wa Kigoma Mhandisi Godwin Mpenzile akitoa maelezo kwa wajumbe wa bodi amesema madaraja matatu ambayo yamejengwa kwa teknolojia ya mawe yamegharimu zaidi ya shilingi milioni 300 kwa ushirikiano wa serikali,and the only nguvu za wananchi na ufadhili wa ubelgiji kupitia shirika la ENABLE   ambalo lilikuwa likitekeleza mradi wa kilimo.