Radio Joy FM

Jamii Kigoma yashauriwa kushirikiana na serikali kukabiliana na uharibifu wa mazangira

20 November 2023, 14:24

Mkuu wa Wilaya Buhigwe Michael Ngayalina akisoma bango la Mradi wa USAID Tumaini kupitia vitendo, Picha na Tryphone Odace

Serikali imesema itaendelea kuthamini mchango wa taasisi ya Jane Goodall katika kuhakikisha inatekeleza shughuli zake za utoaji wa elimu ya mazingira na kilimo kuitia ufadhili wa shirika la Kimarekani la USAID.

Na Tryphone Odace

Wadau wa maendeleo mkoani Kigoma wameshauriwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kukabiliana na uharibifu wa mazangira kwa faida ya viumbe hai.

Hayo yemeelezwa na Mkuu wa Wilaya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye wakati wa uzinduzi wa mradi wa USAID Tumaini Kupitia Vitendo kutoka Taasisi ya Jane Goodall unaoangazia uzalishajiwa kilimo, Uhifadhi wa kudumu wa misitu, kuboresha na kuimarisha haki za ardhi.

Mkuu wa Wilaya Buhigwe akipewa maelezo kwenye bado baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa USAID Tumaini Kupitia Vitendo, Picha na Tryphone Odace

Amesema maliasili nyingi zinaharibiwa kutokana na watu kuendelea kuharibu misitu na maeneo tengufu.

Sauti na Mkuu Wilaya Buhigwe Kigoma

Awali akingumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya Jane Goodall Bw. Jame Lembeli amesema ufadhili usiotosheleza kwenye miradi ya mazingira imekuwa miongoni mwa changamoto zinzosababisha mazingira na misitu kuendelea kuvamiwa na kuharibiwa.

Sauti ya Mjumbe wa Taasisi ya Jane Goodall James Lembeli

Baadhi ya wanafaika wa miradi ya Jane goodall kutoka mikoa ya Kigoma na Katavi wamesema wameweza kupata elimu ya kutosha ya uhifadhi wa mazingira na namna ya kulima kilimo cha mbolea vunde kwa kutumia mbolea ya asili.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa USAID Tumaini Kupitia Vitendo unaotekelezwa na taasisi ya Jane Goodall, Picha na Tryphone Odace

Mradi huu wa USAID Tumaini kupitia Vitendo unatekelezwa kwa Taasisi ya Jane Goodall  na utagharimu dola milioni 28 za kimarekani.