Joy FM

Bajeti iliyopitishwa na madiwani kuchochea maendeleo ya mji kasulu

26 February 2024, 13:26

Baraza la Madiwani wa halmshauri ya Mji Kasulu Mkoani Kigoma limepitisha mapendekezo ya bajeti ya shilingi bilioni 33.3 inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri Kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao cha kupitisha mapendekezo ya bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Picha na Hagai Ruyagila

Hayo yamebainishwa  katika kikao cha robo ya pili ya mwaka cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Mji Kasulu kwa kauli moja wamepitisha bajeti hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Akizungumza baada ya kusomwa bajeti hiyo Kaimu mwenyekiti wa halamshauri ya Mji Kasulu ambaye pia ni diwani wa kata ya Kumnyika Mh. Seleman Kwilusha amesema bajeti hiyo haiwezi kutekelezeka pasipokuwa na umoja na mshikamano kati yao.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Bi. Theresia Mtewele licha ya kulipongeza baraza la madiwani kwa kupitisha bajeti hiyo amesema bajeti hiyo inatafsiri namna ambavyo halmashauri ya Mji Kasulu inasonga mbele katika maendeleo.  

Naye Mwakilishi wa Katibu tawala mkoa wa Kigoma Bi. Jesca Fupi amewasihi madiwani kuhakikisha wanasimamia vyema miradi ya maendeleo iliyopo huku wakimshirikisha mkurugenzi wa hamashauri husika endapo watabaini changamoto katika miradi hiyo.