Joy FM

Kigoma: Mtoto achomwa moto mikono na mama yake kisa muwa

3 July 2023, 10:25

Mtoto mwenye umri wa miaka mitano amechomwa moto mikononi na mama yake mzazi akimtuhumu kuiba muwa.

Mtoto mwenye umri wa miaka mitano akiwa amechomwa moto mikononi , Picha na Hagai Ruyagila.

Na, Hagai Ruyagila.

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Esther Damiani mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa kitongoji cha Uwanjani kata ya Mwandiga halmashauri ya wilaya ya Kigoma amemchoma mikono mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka mitano kwa kutumia mkaa wa moto baada ya kuiba muwa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Tito Mahamudu Kilalika mwenyekiti wa kitongoji cha Uwanjani kata ya Mwandiga amesema baada ya kupewa taarifa walimpeleka mtoto huyo kupata huduma ya kwanza huku taratibu za kumfikisha katika vyombo vya sheria zikiwa zinaendelea.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kitongoji Tito Mahamudu

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Pius Paul wamesema vitendo hivyo sio vizuri kwani vinamfanya mtoto ashindwe kujiamini kutokana na wengi wao kufanyiwa vitendo vya ukatilii wa aina hiyo.

Mashuhuda wa tukio la mtoto kuunguzwa.

Naye Esther Damiani, mama mzazi wa mtoto huyo amesema makosa mengi aliyoyafanya mtoto wake ndiyo sababu iliyopelekea kumchoma mikono ili asiendelee na tabia ya wizi.

Mama mzazi wa Mtoto.

Katibu wa dawati la jinsia katika kijiji cha Mwandiga halmashauri ya wilaya Kigoma Zuhura Kassimu Kasheshe amesema mtoto anapofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili inampelekea kupata tatizo la kisaiklojia huku akibainisha vitendo vya kikatili ambavyo vimesharipotiwa mpaka sasa katika eneo hilo.

Katibu wa Dawati la jinsia Mwandiga.