Joy FM

Aweso amwagiza DC Kibondo kumchukulia hatua mkandarasi

21 July 2023, 09:16

Waziri wa maji akikagua miradi ya maji, Picha na Tryphone Odace

Mkandarasi anayetekeleza mradi wa uchimbaji wa visima vya maji Wilayani Kibondo ametakiwa kukamilisha mradi huo kwa haraka baada ya kutelekeza mradi huo kwa kipindi kirefu na kusababisha wananchi kukosa hudum ya maji.

Na, Kadislaus Ezekiel

Waziri wa maji Jumaa Aweso amemwagiza mkuu wa wilaya ya Kibondo, Kanali Agrey Magwaza, kumuchukulia hatua za kisheria mara moja, mkandarasi aliyepewa tenda ya kuchimba visima vya maji katika vijiji tisa vya Wilaya ya Kibondo, ambavyo havina huduma hiyo, ikiwa atashidwa kuanza kazi ya kuchimba Visima.

Waziri Aweso ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea malalamiko juu ya kero ya ukosefu wa maji, licha ya kuagiza mkandarasi wa kuchimba visima mda mrefu na kukuta kazi hiyo bila utekelezaji.

Sauti ya Mbunge Kibondo na Wananchi wakitoa malalamiko
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua mradi wa maji Wilayani Kibondo, Picha na Tryphone Odace

Hatua hiyo inamlazimu Waziri Aweso kupiga simu kwa mkandarasi huyo na kutoa maelekezo kuanza kazi ya kuchimba visima kwa awamu, katika vijiji tisa ambavyo havina mradi wowote wa maji.

Sauti ya Waziri wa Maji Jumaa Aweso

Ziara ya Waziri aweso mkoani Kigoma, imeacha alama kwa kuchochea kasi ya ukamilishaji wa miradi ya maji.