Joy FM
Joy FM
23 June 2026, 16:19

Teknolojia imeendelea kukua kwa kasi duniani na kuleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali, ikiwemo sekta ya elimu kutokana na maendeleo hayo, walimu wanapaswa kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili waweze kutoa elimu bora inayokidhi mahitaji ya wakati
Na Lucas Hoha
Baadhi ya walimu ambao wameshiriki mafunzo ya namna ya kutumia mifumo ya kidijitali katika kufundisha na kujifunza Mkoani Kigoma ambayo yametolewa na shirika la maendeleo la Ubelgi nchini Tanzania Enabel wamesema mafunzo hayo ya kidajitali yatawasaidia kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kufundisha kwa ufanisi darasani
Wameyasema hayo mara baada ya mafunzo ya siku tatu ambayo yametolewa na shirika la Enabel kupitia mradi wa wezesha BINTI unaotekelezwa na shirika hilo ndani ya Mkoa wa Kigoma
Wamesema kwa sasa dunia imebadilika kutokana na teknlojia hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuendana na ulimwengu wa sasa
Mwakilishi kutoka taasisi ya Elimu Tanzania Dkt Anjela Katabalo amesema shirika la Enabel linatumia gharama kubwa kuweka mazingira wezeshi ya miundombinu itakayosaidia kuinua kiwango cha elimu Mkoani Kigoma.

Kwa upande wake, Meneja wa shirika la Maendeleo la Ubelgiji Enabel Mkoa wa Kigoma anayesimamia mradi wa wezesha BINTI Bi Christin Kalunji amesema mradi huo umelenga kuboresha uelewa kwa walimu na wanafunzi, miundombinu ya kutolea elimu katika Halmashauri tofauti ikiwemo Manispaa ya Kigoma Ujiji

Mafunzo ya kidijitali kwa walimu ni muhimu katika kuimarisha sekta ya elimu na yanawasaidia walimu kuendana na maendeleo ya teknolojia, kuboresha mbinu za ufundishaji na kuongeza kiwango cha elimu kwa wanafunzi. Hivyo, ni muhimu kwa wadau wa elimu kuendelea kuwekeza katika mafunzo na miundombinu ya kidijitali ili kuhakikisha elimu inakuwa sambamba na mahitaji ya karne ya 21.