Joy FM

Tunajivunia muungano kwani maendeleo yapo

25 April 2024, 16:44

Wananchi wakiwa katika mkutano uliondaliwa na mkuu wa wilaya kigoma kujadili umuhimu wa muungano, Picha na Kadislaus Ezekiel

Muungano wa Tanganyika na Zanzabar umeendelea kuwa nguzo ya umoja na mshikamano na kuchochea ukuaji wa maendeleo kupitia utekelezwaji wa miradi mbalimbali wa maendeleo.

Na Kadislaus Ezekiel – Kigoma

Wananchi Mkoani Kigoma, wamepongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga Hospital kubwa pamoja na kutoa fedha nyingi katika miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo Barabara, uwanja wa ndege na ujenzi wa meli katika ziwa Tanganyika.

Wamesema hayo wakati wa zoezi la usafi katika hospitali za mkoa wa Kigoma, ikiwemo Hospital ya Babtist ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa na Viongozi hali ambayo inaelezwa Kuchagiza maendeleo kwa kasi na kuendeleza amani na mshikamao kwa raia wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Sauti ya wananchi wakipongeza serikali na miradi ya maendeleo

Katibu tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Abasi, amesema serikali imefanya kazi kubwa katika sekta ya afya kwa kufanikisha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa na miundombinu bora ya kutolea huduma, wakati Mkuu wa mkoa wa Kigoma aliyewakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Salum Kalli, amesisitiza Muungano kuendelea kuutunza, kuulinda na kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Katibu tawala Mkoa wa kigoma, Picha na Kadislaus Ezekiel
Sauti ya Katibu tawala mkoa wa kigoma na Mkuu wa wilaya kigoma