Joy FM

Wahitimu Kigoma watakiwa kufundisha maadili mema kwenye jamii

10 July 2023, 11:56

Wahitimu wa kada mbalimbali kutoka chuo cha Kigoma Training College katika picha ya pamoja, Picha na Lucas Hoha.

Suala la maadili kwenye jamii limeendelea kuwa changamoto ambapo wahitimu wa vyuo mbalimbali wametakiwa kuwa mfano kwa jamii na kuhimiza maadili ili kuwa na kizazi chenye maadili mazuri.

Na Lucas Hoha.

Wito umetolewa kwa wanafunzi wanaomaliza masomo katika kada mbalimbali kuwa mstari wa mbele katika kuwatetea wananchi na kuifundisha jamii kuwa na maadili mema.

Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki Kigoma, Joseph Mlola amesema hayo wakati wa mahafali ya 22 ya chuo cha Kigoma Training College  KTC kilichopo manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo ameeleza kuwa baadhi ya wasomi wamekuwa hawakemei vitendo viovu hali ambayo imepelekea kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili.

Sauti ya Askofu wa Jimbo la Kathoriki Kigoma Joseph Mlola

Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho Louis  Kusaya amesema  wanachuo ambao wamehitimu masomo yao wamefundishwa maadili kutokana na kada ambazo wamesomea na kuwataka kuwa mfano mzuri kwenye jamii.

Sauti ya Mkuu wa Chuo Kigoma Training College Fr. Louis Kusaga

Baadhi ya wahitimu wa chuo hicho mbali na kutoa shukrani kwa elimu waliyoipata, wamesema watasimamia kile ambacho wamefundishwa darasani ili kuhakikisha wanaisadia jamii kuwa na maendeleo mazuri.

Katika mahafali hayo ya 22 zaidi ya wanachuo 193 wamehitimu masomo yao katika kada mbalimbali ikiwemo uuguzi na ukunga, maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii na  sheria.