Joy FM

Madiwani Kibondo walia na wafanyabiashara wanaoficha mafuta

14 September 2023, 16:58

Baadhi ya madiwani wakiwa katika kikao cha baraza la Madiwani Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma, Picha na James Jovin

Wakati wananchi na watumiaji wa vyombo vya moto Nchi wakiendelea kuteseka na uhaba wa mafuta kwenye vituo vya mafuta huko Kibondo madiwa wameeleza kuwa wanaoficha mafuta ni uhujumu uchumi.

Na, James Jovin

Madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma wameitaka Serikali kupita EWURA kudhibiti wamiliki wa vituo vya Mafuta wenye tabia ya kuficha Mafuta huku wakisubiri bei mpya kwani kufanya hivyo ni kuhujumu uchumi wa nchi.

Madiwani Kibondo wakiwa katika Baraza la madiwani, Picha na James Jovin

Wametoa kauli hiyo wakati wa baraza la madiwani katika halmashauri hiyo ambapo wameeleza kuwa kuzuia au kuficha Mafuta wakati yapo limekuwa likiathiri pakubwa shughuli za usafirishaji.

Mmoja wa madiwani hao bw. Christopher Charles ambaye ni Diwani wa kata ya Kitahana ameitaka serikali kutoa onyo kali kwa wamiliki wa vituo vya Mafuta wenye tabia hiyo ambayo imekuwa ikileta athali kubwa kwa wananchi

Sauti ya Diwani wa Kata ya Kitahana Christopher Charles

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Kanali Agrey  Magwaza  amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kwamba wamiliki hao wanapaswa kufuata masharti ya biashara licha ya kwamba tatizo hilo limeanzia katika mnyororo mzima wa kuleta Mafuta nchini.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Kibondo Mkoani Kigoma Kanali Agrey Magwaza