Joy FM

Waziri Ndalichako atoa wito kuwaandikisha shule watoto wenye ulemavu

18 January 2024, 14:33

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Nchini Tanzania Profesa Joyce Ndalichako amewataka wazazi na walezi Wilayani Kasulu mkoani Kigoma kuwaandikisha shule watoto wao wenye ulemavu ili waweze kupatiwa  elimu itakayo wasaidia kutimiza ndoto zao.

Na, Trphone Odace

Prof. Joyce ndalichako ambaye pia ni mbunge wa jimbo la kasulu Mjiji amesema hayo wakati akizungumza na wananchi mjini Kasulu ambapo amesema kuwa watoto wenye ulemavu wanahaki ya kupata elimu sawa na watoto wengine.

Ndalichako amesema serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwa ajili  ya kuwawezesha watoto wenye ulemavu waweze kupatiwa elimu katika mazingira mazuri.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Isaac Mwakisu amesema hajaridhishwa na mwenendo wa namna watoto wanavyoripoti shuleni tangu shule zilipofunguliwa januari 8 mwaka huu.

Hata hivyo Baadhi ya wananchi katika halmashauri ya mji kasulu Sylevanus Edwin na Joan Jofrey wamesisitiza kwa wazazi na walezi kuendelea kuwaandikisha watoto wao kupata elimu ya msingi na awali pamoja na kuwapeleka shule waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza