Joy FM

Wananchi Kimobwa watakiwa kuzingatia lishe bora kwa watoto

12 March 2024, 13:21

Afisa lishe Kutoka Hospitali ya Wilaya Kasuluakitoa elimu ya lishe kupitia siku ya lishe ya Mtaa, Picha na Emmanuel Kamangu.

Jamii mkoani Kigoma imetakiwa kuzingatia matumizi ya vyakula vyenye lishe kwa watoto ili kusaidia kuwakinga na utapiamlo ambao unasababisha udumavu kwa watoto.

Na, Emmanuel Kamangu

Wananchi wa kata ya Kimobwa halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kuendelea kuhudhuria kikamilifu siku ya lishe ya mtaa ili kupewa elimu ya makundi bora ya vyakula vinavyotakiwa kwenye lishe ya watoto.

Hayo yameelezwa na Afisa Lishe kutoka hospital ya wilaya Kasulu Bi. Rehema Stephano wakati wa siku ya lishe ya mtaa wa Kimobwa ambapo amewataka wananchi kuhakikisha wanazingatia lishe bora ili kukabiliana na udamavu pamoja na utapia mlo kwa watoto.

Sauti ya Afisa lishe wilaya ya Kasulu

Kwa upande wake, afisa mtendaji kata ya Kimobwa B. Sifa Evaristo amewataka wananchi wa kata hiyo kutumia vema elimu ya lishe bora ambayo wamepewa ili kuzisaidia familia zao kuwa na afya njema.

Sauti ya afisa Mtendaji wa kata ya Kimobwa

Aidha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Koku Gonza ambaye ni mkaguzi kata ya Kimobwa amewataka wananchi kuacha tabia ya kutoa fedha kuwapa kamchape badala yake watumie fedha hizo kununua vyakula vitakavyo wasaidia kupata mlo kamili.

Wananchi ambao wameshiriki mafunzo hayo wamesema kwa kiasi kikubwa wamepata uelewa wa makundi sahihihi ya vyakula vinavyoweza kuwasaidia kuwa na afya njema.

Wananchi wa kata ya Kimobwa wakipata elimu ya lishe, Picha na Emmanuel Kamangu

Mafunzo hayo yametawaliwa na majiko darasa ambapo kila mwananchi amejifunza kwa vitendo jinsi ya kupika vyakula vye lishe bora.