Joy FM

Madereva watakiwa kuongeza umakini msimu huu wa mvua zinazoendelea kunyesha

1 January 2024, 14:03

Madereva wa mabasi yaendayo mikoani wametakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani hasa kipindi hiki cha mvua ili kudhibiti athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo ajali.

Mkuu wa dawati la elimu usalama barabarani ,ACP Michael Dereri akikagua moja ya mabasi yaendayo mikoani. Picha Na Josephine Kiravu

Na Josephine Kiravu.

 Akizungumza na madereva Mkuu wa dawati la elimu usalama barabarani Nchini, ACP Michael Dereri amesema ajali nyingi ambazo zimekuwa zikijitokeza kutokana na uzembe wa madereva pamoja na uchakavu wa baadhi ya vifaa kwenye baadhi ya mabasi.

Sauti :Michael Dereri.

Nao baadhi ya madereva wa mabasi akiwemo Yusuph Mzigua wameshukuru kwa elimu waliyopatiwa huku wakilitaka jeshi la polisi kuona namna ya kuwawajibisha wamiliki ambao wamekuwa wanalazimisha mabasi yenye hitilafu kuingia barabarani.

Sauti :Madereva

Nao abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea mikoa mbalimbali hapa nchini akiwemo Josephine Kavano wameeleza faida za jeshi la polisi kufanya ukaguzi wa mabasi kabla ya kuanza safari huku wakitaka ukaguzi huo kuwa endelevu.

Sauti :Abiria

Mwishoni mwa wiki iliyoisha Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani walifanya ukaguzi wa mabasi yaendayo mikoani zaidi ya 20 na kubaini mapungufu kwenye mabasi 3 ambayo yalitozwa faini huku basi moja likizuliwa kabisa kuendelea na safari hadi uakarabati utakapofanyika.