Joy FM

Wananchi walalamikia ubovu wa stendi ya mabasi Kibondo

15 April 2024, 12:37

Wananchi pamoja na Madereva wa vyombo vya moto Wilayani Kibondo mkoani Kigoma, wamelalamikia ubovu wa miundombinu ya stendi ya mabasi wilayani humo, hali inayopeleeka kukwama vyombo vya moto vikiwa stendi hasa kipindi cha masika, na kuomba hatua za halaka zichukuliwe ikiwemo kuboresha miundombinu pamoja na njia za kutoka na kuingia.

Wakizungumza na Radio Joy, baadhi ya wananchi na madereva wamesema mvua zinaponyesha shughuli za usafirishaji zinalazimika kukwama kutokana na tope linalokuwepo ndani ya stendi ya mabasi huku shughuli za uzalishaji mali zikilazimika kisimama.

Akiwa katika mkutano wa hadhara mbunge wa jimbo la mhambwe wilayani kibondo daktari frorence samizi, amesema serikali tayari imetoa kiasi cha milioni mianne ili kuanza ujenzi wa miundombinu ya stendi ya wilaya ya kibondo, na kuahidi kuendelea kufanya ufatiliaji ili stendi hiyo ikamilike.