Joy FM

Serikali kutumia bilioni 40 kukarabati meli mbili ziwa Tanganyika

29 November 2023, 09:57

Serikali inatarajia kutumia jumla ya Shilingi Bilioni 40 kukarabati meli kongwe ya abiria na mizigo ya MV Liemba pamoja na meli ya mafuta ya MT Sangara yenye uwezo wa kubeba lita laki nne za mafuta ambayo  matengenezo yake  tayari yameanza.

Akizungumza baada kutembelea na kukagua shughuli za Kampuni ya Huduma za Meli nchini MSCL, Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, ameiagiza kampuni hiyo, kuhakikisha ukarabati wa meli ya mafuta ya MT Sangara unakamilika mapema hapo mwakani.

Sauti ya Naibu waziri wauchukuzi David Kihenzile.

Amesema  ukarabati na ujenzi wa meli mpya za Ziwa Tanganyika vina uhusianno wa moja kwa moja na uwekezaji mkubwa katika bandari ya Dar es salaam ambao utawezesha nchi kunufaika na fursa ya soko la nchi za jirani.

Sauti ya Naibu waziri wauchukuzi David Kihenzile.

Kaimu Meneja wa MSCL tawi la Kigoma Allen Butembero, amesema ukarabati wa meli ya MT Sangara umefikia asilimia 92% na kwamba unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi aprili mwaka ujao huku akieleza mpango wa ukarabati wa meli ya mv liemba.

Kaimu Meneja MSCL tawi la Kigoma.

Kwa miaka mingi wakazi wa ukanda wa Ziwa Tanganyika hususani wa mkoa wa kigoma, walitegemea sana meli kongwe ya MV Liemba kwa usafiri wa majini huku meli ya mafuta ya MT Sangara ikitegemewa sana na nchi za jirani kwa ajili ya kusafirisha shehena ya mafuta.

Hata hivyo meli ya MV Liemba imesimama kutoa huduma tangu mwezi oktoba mwaka 2018 huku meli ya MT Sangara pia ikisimama kutoa huduma tangu mwezi mmwaka 2020 kutokana na uchakavu.