Joy FM

FAO kuinusuru kigoma dhidi ya Magonjwa ya mlipuko

23 April 2024, 13:19

Serikali kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO, imeanza kuchukua hatua kukabilina na magonjwa ya mlipuko kwa mikoa inayopakana na nchi jirani, hasa magonjwa yatokanayo na wanyama, ili kulinda afya ya binadamu, mifugo na mazingira. 

baadhi ya wadau wa Afya mkoani Kigoma wakiwa katika kikao cha kujadili namna ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. Picha na kadislaus Ezekiel

 Na Kadislaus Ezekiel.

Mratibu wa mradi wa kudhibiti Usugu wa vimelea vya magonjwa kutoka shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO Daktari Eribalick Mwakapeje amesema magonjwa ya mlipuko yamekuwa hatari kwa binadamu na kuhatarisha usalama.

Sauti yake Eribalick Mwakapeje

Katibu Tawala mkoa wa Kigoma Hassan Abas amesema kutokana na mwingiliano wa raia kutoka nchi jirani, mikoa ya mipakani iko kwenye hatari ya magonjwa ya mlipuko, Wakati mkuu wa mkoa wa Kigoma aliyewakilishwa na mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salumu Kalli akisisitiza maeneo ya mpakani kudhibitiwa kubaini athali za magonjwa ya mlipuko.

Sauti yake Hassan Aba – katibu tawala mkoa wa Kigoma