Joy FM

Kibondo hakuna mafuriko lakini kuna athari kubwa

12 January 2024, 08:37

Licha ya kutokuwepo mafuriko katika wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma lakini mvua zinazoendelea kunyesha zimeacha athali mbali mbali ikiwemo uharibifu wa miundo mbinu ya barabara, uharibifu wa mazao shambani na kuezuliwa kwa nyumba. 

Na, James Jovin

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Kibondo kanali Agrey Magwaza wakati akizungumza na radio Joy ofisini kwake na kwamba wananchi wanapaswa kuchukua tahadhali kubwa wakati huu ambao mvua kubwa zinaendelea kunyesha.

Aidha amesema kuwa kamati ya maafa ya wilaya inaendelea kufanya tathimini mbali mbali ya madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha lakini pia kutoa elimu kwa wananchi ya namna ya kujikinga na madhara ya mvua

Katika hatua nyingine bw. Magwaza amewataka wakala wa barabara vijijini Tarura pamoja na Taniroads kukagua barabara mbali mbali na kuzifanyia matengenezo ili ziweze kuwasaidia wananchi katika shughuli zao.