Joy FM

Wazazi kushirikiana tiba ya upendo kwa mzazi mmoja

8 January 2024, 16:43

Baadhi ya wazazi wakiume wilayani Kasulu Mkoani Kigoma wametakiwa kushirikiana na wazazi wa kike kuzilea familia zao na kuacha kuzitelekeza hali inayopelekea baadhi ya watoto kuwa na mapenzi na mzazi mmoja.

Rai hiyo imetolewa na Mchungaji kiongozi wa kanisa la full gospel bible fellowship Mike Kiwale lililopo katika halmashauri ya Mji Kasulu wakati wa ibada takatifu ya jumapili.

Mch. Kiwale amesema wazazi wengi wa kiume wamekuwa wakiwaachia majukumu wake zao hali inayopelekea matabaka kwa watoto kutokana na kulelewa na mzazi mmoja.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi wakiume wamekili kutokea kwa hali hiyo huku wakisema mchungaji amewakumbusha kutimiza wajibu wao kwa familia ili kuondoa changamoto katika familia zao.

Emiliana Gabriel ni mzazi wakike aliyeachiwa familia ili kuwalea watoto wake ambaye amesema akina mama hawatakiwi kukata tamaa badala yake wamuombe Mungu maana yeye ndiye anaweza kuwasaidia katika changamoto

.