Joy FM

DC kasulu atangaza vita wazazi kuzuia watoto kwenda shule

12 December 2024, 12:51

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu ameliagiza baraza la madiwani la halmashauri ya Mji Kasulu mkoani Kigoma kuhakikisha wanafuatilia watoto wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa ili kuanza elimu ya awali na msingi na wale waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu wakati akihutubia kwenye kikao Cha Baraza la madiwani Cha halmashauri ya Mji Kasulu Cha robo ya kwanza ya Mwaka 2024/25.Picha na Hagai Ruyagila

Kanal Mwakisu amebainisha hayo katika kikao cha baraza la madiwani cha robo ya kwanza ya mwaka 2024/25

Amesema ni jukumu la kila diwani kwenye kata yake kuhamasisha wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wao ifikapo mwezi januari 2025.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanal Isaac Mwakisu

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl, Vumilia Simbeye amesema amepokea maelekezo hayo na atahakikisha anayafanyia kazi sambamba na kusimamia miradi ya maendeleo inayopelekwa na rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika halmashauri hiyo

Mwl, Vumilia Simbeye

Naye Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Seleman Kwirusha amesikitishwa na ukusanyaji wa mapato ndani ya halmashauri hiyo ambapo amewaagiza madiwani wote kuhakikisha wanasimamia vyema mapato katika kata zao.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kasulu Seleman Kwirusha
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl Vumilia Simbeye. Picha na Hagai Ruyagila

..