Joy FM

DC Kasulu ataka wananchi kuenzi muungano

27 April 2026, 12:17

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akipanda mtu katika maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar shule ya msingi kimobwa, Picha na Hagai Ruyagila

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni moja ya matukio muhimu zaidi katika historia ya Tanzania, ulioweka msingi wa taifa moja lenye umoja, amani na mshikamano na Muungano huu ulianzishwa tarehe 26 Aprili 1964, ukiziunganisha nchi mbili zilizokuwa huru kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Na Hagai Ruyagila

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Isaac Mwakisu, amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuendelea kudumisha na kuuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ili kuimarisha amani iliyopo nchini.

Kanali Mwakisu ametoa wito huo wakati wa zoezi la upandaji miti lililofanyika katika Shule ya Msingi Kimobwa Halmashauri ya Mji Kasulu, ambapo jumla ya miti 150 imepandwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akipanda mtu katika maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar shule ya msingi kimobwa, Picha na Hagai Ruyagila

Amesisitiza umuhimu wa Muungano huo kwa maendeleo ya taifa, na kueleza kuwa utunzaji wa mazingira ni msingi muhimu kwa ustawi wa maisha ya wananchi.

Sauti ya Kanali Isaac Mwakisu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Kasulu, Mbelwa Chidebwe amesema wao kama Chama Cha kilichopo madarakani, wataendelea kuisimamia serikali iendelee kudumisha Muungano.

Baadhi ya viongozi wa CCM wakipanda miti, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Mbelwa Chidebwe

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl.Vumilia Julius Simbeye amesema upo umuhimu mkubwa wa kuuenzi Muungano ulioasisiwa na viongozi wetu.

Sauti ya Mwl. Vumilia Simbeye
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye akipanda mtu katika maadhimisho ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Picha na Hagai Ruyagila

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kimobwa ameahidi kusimamia na kuitunza miti hiyo ili iweze kusaidia kuboresha mazingira ya shule.

Sauti ya Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kimobwa