Joy FM

Mtoto aliyechomwa moto mikoni kwa kuiba muwa apata matibabu

27 July 2023, 10:58

Kufuatia mtoto wa miaka mitano kuchomwa moto mikono na mama yake mzazi Esther Damiani mnamo tarehe Juni 29 mwaka huu baada ya kuiba muwa, hatimaye mtoto huyo anaendelea vizuri kutokana na matibabu anayoendelea kupatiwa.

Na, Hagai Ruyagila.

Akizungumza na Radio Joy FM, Zuhura Kassimu Kasheshe Katibu wa Dawati la jinsia kata ya Mwandiga amesema maendeleo ya mtoto huyo yanatia moyo kutokana na matibabu anayoendelea nayo.

Mkono wa mtoto aliyechomwa na mama yake ukiwa na makovu baada ya kupatiwa huduma, Picha na Hagai Ruyagila
Sauti ya Katibu wa Dawati la jinsia kata ya mwandiga

Bi. Zuhura Kasheshe amewasihi wazazi na walezi wa kata hiyo kudhibiti hasira wanazokuwa nazo baada ya watoto kufanya vitendo ambavyo haviwapendezi ili kutosababisha madhara ndani ya familia na katika jamii inayowazunguka.

Sauti ya Katibu wa Dawati la jinsia Kata ya mwandiga

Hata hivyo Radio Joy FM imezungumza na Tito Mahamudu Kilalika mwenyekiti wa dawati la jinsia  kata ya Mwandiga na mwenyekiti wa kitongoji cha Uwanjani ili kujua kama elimu ya ukatili inatolewa kufuatia matukio hayo ya ukatili kujirudia mara kwa mara.

Muonekano wa aliyechomwa moto na mama yake mzazi
Mwenyekiti wa dawati la jinsia kata ya mwandiga Kigoma

Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo Esther Damiani aliyemfanyia ukatili huo mtoto wake amesema, hatorudia kufanya ukatili wa aina yoyote na kwa mtu yeyote kutokana na madhira ambayo ameyaona mtoto wake akipitia kipindi akipatiwa matibabu.

Sauti ya mama mzazi ambaye ndiye aliyemchoma moto mikoni mtoto wake

Ni takribani siku ishirini na nane zimepita tangu mtoto huyo alipofanyiwa ukatili wa kinjinsia na mama yake mzazi baada ya kuiba muwa wenye thamani ya shilingi 200/= katika mtaa wa Uwanjani ndani ya kata hiyo.