Joy FM

Wananchi waomba serikali kupunguza gharama nishati safi

10 October 2024, 14:27

Muonekano wa mitungi ya gesi kutoka kampuni mbalimbali, Picha na The chanzo

Serakali imeendelea kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kupunguza uharibifu wa mazingira.

Na Tryphone Odace – Kigoma

Wananchi mkoani Kigoma wameiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za ununuzi wa majiko ya nishati safi ikiwemo gesi na jiko la umeme ili kuhama kuoka matumizi ya Kuni na mkaa wa kupikia ambayo inatajwa kuharibu mazingira na kikwazo kiafya huku wadau wengine wakipendekeza kutumika mfumo wa ruzuku katika manunuzi ili kupunguza ukali wa gharama. 

Nishati safi ya kupikia imetajwa kuwa nyenzo muhimu ya kusaidia kuepusha uharibifu wa mazingira Pamoja na kuisaidia jamii kujiepusha na matatizo ya kiafya kutokana na uchafuzi wa hali ya hewa ndani nyumba Kwa matumizi ya kuni na mkaa wakati wa kupikia.

Katika kuhakikisha Mazingira yanatunzwa na afya zinalindwa serikali ilianzisha mpango wa nishti safi ambao utawawezesha watanzania kujiepusha wakati mwingine na migogoro na
mamalaka zinazosimamia misitu. 

Wajasiliamali kwa niaba ya Jamii nyingine hasa maeneo ya vijijini wameiomba serikali kuona umuhimu wa kusaidia kupunguza gharama za majiko hayo ya nishati safi ya kupikia.

Sauti za wajasiliamali wa Mkoa wa kigoma

 
Hatua hiyo imejiri wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Mapishi safi mkoani Kigoma kwa kutumia Nishati safi ya kupikia inayotekelezwa na shirika la UNIDO

Akizunguma Meneja Utafiti kutoka Tanesco Mhandisi Samweli Kessy ameeleza namna nishati ya umeme ilivyo na faida wakati wa kupikia huku mwakilishi wa Banki ya maendeleo ya TIB nchini Andrew Mwampaghale ameeleza umuhimu wa kutumia Ruzuku ili kupunguza gharama za ununuzi wa majiko hayo.

Sauti ya Meneja Utafiti kutoka Tanesco Mhandisi Samweli Kessy

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye amesema matumizi ya nishati safi ya umeme itasaidia kuokoa muda katika upishi na kuimarisha afya.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali mstaafu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Thobias Andengenye