Joy FM

Jeshi la Polisi limetoa msaada kwa wagonjwa Kasulu

31 July 2026, 16:02

Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoa wa kigoma, Alfred Kasolo katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi wilaya ya Kasulu katika hospital ya Mlimani Mjini Kasulu, Picha na Hagai Ruyagila

Msaada huo ni sehemu ya Jshi hilo kuendelea kuimarisha ukaribu na ushirikiano kwa jamii

Na Hagai Ruyagila

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma limetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni, mafuta ya kujipaka na kanga nguo, kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mlimani iliyopo Halmashauri ya Mji Kasulu, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Kamishna Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa upelelezi na makosa ya jinai mkoa wa kigoma Alfred Kasolo, amesema Jeshi la Polisi ni sehemu ya jamii, hivyo limeona umuhimu wa kurejesha shukrani kwa wananchi linaowalinda kwa kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini.

Sauti ya Alfred Kasolo
Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoa wa Kigoma, Alfred Kasolo, Picha na Hagai Ruyagila

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mlimani, Editha Yohana Vubuka, ambaye pia ni Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, amesema msaada huo utasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zinazowakabili wagonjwa na hospitali kwa ujumla. Aidha, amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuonyesha upendo na huruma kwa wagonjwa kupitia msaada huo.

Sauti ya Daktari Mlimani
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mlimani, Editha Yohana Vubuka, ambaye pia ni Muuguzi Mfawidhi wa hospitali hiyo, Picha na Hagai Ruyagila

Baadhi ya wagonjwa waliopokea zawadi hizo wameeleza kufurahishwa na hatua ya Jeshi la Polisi ya kuwafikia na kuwapa zawadi hizo, wakisema kitendo hicho kinaonyesha kuwa jeshi hilo linathamini na kushirikiana na jamii hata katika nyakati za matatizo.

Sauti ya Ndugu wa Mgonjwa
Askari Polisi akikabidhi zawadi kwa mgonjwa, Picha na Hagai Ruyagila