Joy FM
Joy FM
26 August 2026, 15:54

Malezi bora ya watoto ni jambo muhimu katika maisha ya kila mtoto na malezi huanzia nyumbani kwa huhusisha namna wazazi au walezi wanavyomlea, kumlinda, kumfundisha au kumpa mahitaji muhimu, mtoto anayepata malezi bora huwa na nafasi kubwa ya kukua akiwa na afya njema, tabia nzuri na uwezo wa kuishi vizuri na watu wengine
Na Sofia Cosmas
Wazazi na walezi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wametakiwa kuzingatia malezi ya watoto na kufuatilia mienendo na tabia zao ili kuwajenga katika misingi ya maadili mema na yanayokubalika katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwalimu Colineli Kisinga amesema wazazi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wao wanapata malezi bora, kwa kuwa malezi bora ndiyo msingi wa kuwa na jamii yenye maadili.
Amesema hayo katika mahafali ya darasa la Saba yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Cambridge Shire, iliyopo Businde Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa shule hiyo, Bi. Betha Buganga, amewataka wazazi kuendelea kuwa karibu na watoto wao na kuwapatia ushauri unaofaa, hasa wanapofikia kipindi cha balehe.
Awali, katika risala iliyowasilishwa kwa mgeni rasmi, uongozi wa shule umeeleza kuwa moja ya changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo ni ubovu wa barabara ya Buhanda–Businde, hali inayosababisha barabara hiyo kutopitika kwa urahisi.
Kwa upande wao, baadhi ya wazazi wameitaka jamii kumweka Mungu mbele katika malezi ya watoto wao.

Hata hivyo, Kisinga ameahidi kulichukua kwa uzito suala la ubovu wa barabara hiyo na kuhakikisha changamoto hiyo inafanyiwa kazi.
Mahafali hayo ni ya tano kufanyika tangu kuanzishwa kwa shule ya Msingi Cambridge