Joy FM

Miradi 7 ya zaidi ya bilioni 15.4 kuzinduliwa na mwenge wa uhuru Buhigwe

11 September 2026, 11:46

Mkuu wa Wilaya Kasulu Kanali Isaac Mwakisu akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Wilaya Buhigwe, Picha na Hagai Ruyagila

Mwenge wa uhuru umeendelea kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Mkoa wa Kigoma huku ukisisitiza miradi hiyo kutunzwa

Na Hagai Ruyagila

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake leo Septemba 11, 2026 katika Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, ukitokea Wilaya ya Kasulu, ambapo unatarajiwa kuzindua, kutembelea, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akisoma taarifa kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mganasha wilayani Buhigwe, Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Michael Ngayalina, amesema Mwenge huo utakimbizwa umbali wa kilomita 54 na kuzindua na kutembelea jumla ya miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 15.4

Mkuu wa Wilaya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina akizungumza wakati wa mwenge wa uhuru ulipowasili Wilayani humo, Picha na Hagai Ruyagila

Kanali Ngayalina amesema miradi hiyo inahusisha sekta mbalimbali, ikiwemo elimu, huku baadhi ikizinduliwa, mingine ikitembelewa na kukaguliwa, pamoja na kuwekwa mawe ya msingi.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Buhigwe wamesema Mwenge wa Uhuru umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi, hususan katika kuhamasisha maendeleo, uzalendo, amani na mshikamano katika jamii.

Baadhi ya wananchi wakiwa katika mapokezi ya mwenge wa uhuru 2026, Picha na Hagai Ruyagila